MAFUNZO YA TAHADHARI KWA MABWAWA YATAFANYIKA JIJINI MWANZA NOVEMBA, 2025

Na Mwandishi wetu Dodoma

Tanzania ni miongini mwa Nchi ambazo zimeshuhudia majanga yatokanayo na mabwawa ya maji na tope sumu yanapobomoka, na si jambo geni kwani pia limekuwa likiripotiwa na vyombo vya habari katika nchi ambazo zimekubwa na majanga makubwa yatikanayo na kubomoka kwa mabwawa hususan ya tope sumu.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Diana Kimario ambaye pia ni Mkurugenzi Tathmini na ufuatiliaji ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma katika Mkutano na Waandishi wa habari ambapo amesema Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Chemba ya Migodi Tanzania pamoja na watalaam wa Kampuni ya Uhandisi ya City wameshirikiana kuandaa mafunzo ya siku tatu (3) yatakayoshirikisha wataalam kutoka Sekta binafsi na Serikalini ikiwamo wamiliki wa migodi kwa ajili ya usalama wa mabwawa ya majisafi na tope sumu (TSF).

Mafunzo hayo yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Novemba 19-21, 2025 yakiwa na kaulimbiu isemayo ‘Tahadhari za dharura za Kukabiliana na Majanga ya Mabwawa ya Maji na Tope sumu.’

Diana amesema mafunzo hayo hufanyika kila mwaka na mwaka 2025 ni mara ya tatu mfululizo ambapo mafunzo yamekuwa na mchango chanya katika kujenga uelewa wa namna bora ya kukabiliana na matatizo yanayotokana na mabwawa yakiwemo mabwawa ya tope sumu.

Pia mafunzo hayo yamekuwa yakijumuisha wataalam waliobobea kutoka mataifa yaliyoendelea kwenye eneo linalohusu usalama wa mabwawa jambo ambalo limewezesha ufanisi wa mabwawa na kuepusha changamoto zinazosababishwa na mabwawa, na kusisitiza kuwa Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaamini katika ushirikishwaji wa wadau wa sekta binafsi hivyo Wizara ya Maji itaendelea kuwa karibu na wadau hao ili kuhakikisha malengo yanafikiwa.

“Ni wajibu wetu sisi kama Serikali kuhakikisha tunalinda usalama wa Wananchi na mali zao na ndiyo maana tunaandaa Mikutano kama hii inayoshirikisha wadau ili sote tuweze kuwa na uelewa kwa pamoja kuhusu hatua na dharura za kuchukua zinapotokea ajali za kubomoka kwa mabwawa”.

Hata hivyo Diana amewataka wadau wote wa mabwawa ndani na nje ya nchi kujitokeza kujiandikisha ili kushiriki mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Migodi Tanzania (Tanzania Chamber of Mines-TCM) Mhandisi Benjamini Mchwampaka ameipongeza serikali kwa jinsi ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu.

Amesema wataendeela kuwa pamoja ili kuhakikisha sekta ya maji na madini kwa ujumla zinakuwa na kuifikia jamii na kusisitiza kuendelea kuwatumia wataalam mbalimbali kuwapa ujuzi watanzania katika kuhakikisha kuwa mabwawa ya maji na yale ya tope sumu yanakuwa salama muda wote.


Related Posts