Rais mstaafu Buhari azikwa, maelefu wajitokeza kumuaga barabarani

Rais wa zamani wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amezikwa jana Jumanne Julai 15, 2025 katika mji wake wa nyumbani wa Daura, Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria, ambako maelfu ya watu walijitokeza barabarani kumuaga.

Buhari alifariki Jumapili  Julai 13, 2025  akiwa London nchini Uingereza, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mara ya kwanza alishika madaraka mwaka 1983 katika taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika, baada ya mapinduzi ya kijeshi aliongoza kwa mtindo wa kiimla hadi alipoondolewa madarakani na wanajeshi wenzake ndani ya miezi 20 baadaye.

Alichaguliwa tena mwaka 2015, akiwa mgombea wa upinzani wa kwanza kushinda uchaguzi wa urais nchini humo.

Katika uchaguzi huo, Buhari alipata ushindi mkubwa kutokana na ahadi yake ya kukomesha rushwa na kuimarisha hali ya usalama Nigeria.


Aliiongoza nchi hiyo hadi mwaka 2023, katika kipindi kilichojaa ghasia kutoka kwa kundi la kigaidi la Boko Haram Kaskazini-Mashariki na hali mbaya ya kiuchumi.

Related Posts