Balla Conte Atua Dar, Kukamilisha Dili na Yanga – Global Publishers



Kiungo chipukizi wa CS Sfaxien ya Tunisia, Mussa Balla Conte

Kiungo chipukizi wa CS Sfaxien ya Tunisia, Mussa Balla Conte (21), anasemeka kutua nchini Tanzania mapema asubuhi ya leo kwa ajili ya kukamilisha usajili wake na miamba wa soka la Tanzania, Yanga SC.

Conte, ambaye pia alikuwa kwenye rada za Simba SC, ametua akitokea Tunisia na kupokelewa na viongozi wa Yanga SC kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho kabla ya kusaini mkataba rasmi.

Nyota huyo anatajwa kuwa mmoja wa viungo wenye kipaji kikubwa na uwezo wa kucheza kama kiungo wa kati au mkabaji, na Yanga SC wanaamini atakuwa nyongeza muhimu katika kikosi chao kuelekea msimu wa 2025/26.