KIUNGO aliyemaliza mkataba Tanzania Prisons, Berno Ngassa amewataja wachezaji wanne aliyokuwa anawatazama kama mfano wa kuigwa wanavyocheza kimbinu na akili msimu uliyopita.
Ngassa ambaye msimu uliyopita alimaliza na mabao manne na asisti moja alisema kutoka Prisons Haruni Chango (mabao manne, asisti moja) wa Yanga Maxi Nzengeli (mabao sita sita, asisti 10), Pacome Zouzoua (mabao 12, asisti 10) na Simba ni Elie Mpanzu (mabao manne, asisti sita) ni wachezaji mafundi wa mbinu uwanjani ambao wana uwezo wa kuzibeba timu zao.
“Wachezaji hao wana ufundi mkubwa sana uwanjani, jinsi ambavyo wanatoa pasi zao kwa akili, kuficha mipira mguuni, wanajua nini wakifanye pindi timu zao zinapokuwa zinazidiwa na wapinzani,” alisema Ngassa na kuongeza;
“Mfano Chanongo nilikuwa nafaidi uchezaji wake wakati wa mazoezi anacheza kiufundi hadi kocha alikuwa anafurahishwa na kuna muda alikuwa ananielekeza kipi nikifanye ili niwe mchezaji mzuri.” Ngassa anayetajwa kusaini Dodoma Jiji, alisema msimu unaokuja anaona utakuwa na mabadiliko makubwa kiuchezaji, kutokana na kujifunza vitu vingi uliyopita wa 2024/24 ambavyo anavifanyia kazi kwa sasa.
Kwa upande wa Chanongo alimzungumzia Ngassa: “Ni mchezaji mzuri sana, nilichokuwa namshauri azingatie ni nidhamu ili kipaji chake kimlipe, akifanye hivyo naamini atafika mbali.”