Nyota wa Simba, Debora Fernandes Mavambo naye ameaga na kwamba hatokuwa kwenye kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao 2025/26.
Mavambo alijiunga na Simba msimu wa 2024/25 kwa miaka mitatu na hivyo ametumikia mwaka mmoja pekee.
Mavambo ameaga rasmi kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram ambapo ameandika:
“Tangu mwanzo kama mchezaji mchanga hadi nyakati za furaha uwanjani, nilipata uzoefu wa ajabu ambao ulinijenga kama mtu na kama mwanasoka”.
“Nitakumbuka mazoezi, mechi na nyakati nilizoshiriki na wachezaji wenzangu, lakini ninafuraha kwa matukio mapya yanayoningoja.”
“Nawashukuru sana familia ya Simba kwa sapoti yenu katika kipindi chote nilichokuwa ndani ya klabu hii, pamoja na wapenzi na viongozi wote wa Simba Sport Club Tanzania”.
Mavambo anakuwa mchezaji wa saba kuaga Msimbazi, baada ya wengine sita ambao ni Frabrice Ngoma, Aishi Manula, Valemtine Nouma, Hussen Kazi, Augustine Okejepha na Kelvin Kijili kuagwa klabuni hapo.
Akiwa Simba, Mavambo ameondoka na medali ya ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya RS Berkane.