::::::::::
Na Ester Maile
Uzalishaji wa Pamba hai katika
Mkoa wa Simiyu umeongezeka kutoka Tani 10,300 mwaka 2021/2022 hadi Tani 12,285 mwaka 2022/2023, jambo lililopelekea Tanzania kuingia katika ramani ya uzalishaji duniani.
ameyasema hayo hii leo Julai 18, 2025 Jijini Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anamringi Macha wakati akizungumza na Watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari, kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita .
Aidha Macha ameongeza kuwa Tanzania ilishika nafasi ya saba (7) na ya Tano (5) mtawalia katika uzalishaji wa Pamba hai ikitanguliwa na Nchi za China, India, Uturuki na Tagekistani.
Amesema, “asilimia 80 ya Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wanategemea Kilimo, katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 Mkoa uliendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha Sekta hiyo na kupata mafanikio makubwa.”
Macha ameongeza kuwa, jumla ya Shilingi Bilioni 89.34 zimepokelewa kwa ajili kutekeleza miundombinu ya kuboresha huduma ya Maji, ambapo Shilingi Bilioni 63.73 zimetumika kutekeleza Miradi 85 ya Maji vijijini huku Shilingi Bilioni 25.61 zimetumika kutekeleza Miradi 61 katika miji ya Bariadi, Maswa, Busega na Meatu ambayo yote imekamilika na inatoa huduma.