POCHI YA RAIS SAMIA YAFUNGUKA//BIL 98.893 KUIMARISHA ELIMU YA SEKONDARI MBEYA NA MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 98.893 kwa ajili ya kuimarisha sekta ya elimu katika mkoa wa Mbeya na Mtwara.

Fedha hizo zimetolewa kupitia Mradi wa kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari-SEQUIP kwa ajili ya kukarabati shule kongwe, kujenga shule mpya, madarasa, nyumba za walimu, na matundu ya vyoo katika shule za Sekondari.

Katika mkoa wa Mbeya tangu mwaka 2022 hadi 2024 jumla ya shilingi Bilioni 24,531,200,420.00 zimetolewa kwa ajili ya kujenga shule mpya 22 za sekondari za kata, ujenzi na shule ya sekondari ya Wasichana ya Bweni, Ukarabati wa shule ya Sekondari Mwakaleli, na umaliziaji wa maabara.

Vilevile, ukamilishaji wa madarasa, na matundu 221 ya vyoo, nyumba 8 za walimu, Shule 2 za Amali, Upanuzi wa shule 6 za sekondari ziwe za kidato cha tano na kuongeza mabweni ya shule, kujenga madarasa, Ukamilishaji wa miundombinu katika shule maalumu ya Wasichana ya Mkoa iliyojengwa Wilayani Kyela.

Katika mkoa wa Mtwara serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 74.362 kupitia mradi wa SEQUIP kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya 38, nyumba 21 za walimu, Mabweni 29 na vyoo matundu 137, Madarasa 20, Madarasa 26, na Maboma ya madarasa 27.