VIDEO: Uteuzi wagombea ubunge, udiwani CCM kufanyika Julai 28

Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa kikao cha Kamati Kuu kwa ajili ya kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu uteuzi wa watia nia wa ubunge na udiwani kitafanyika Julai 28, 2025.

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 19, 2025, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi, Amos Makala, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Makala amesema kikao hicho cha Kamati Kuu kitaamua ni wagombea gani watakaopitishwa kwenda kupigiwa kura za maoni na wajumbe wa CCM, kabla ya kusimamishwa rasmi na chama hicho kugombea ubunge.



CCM yaanika tarehe rasmi ya kuteua wagombea ubunge, udiwani

Ameeleza kuwa awali vikao vya Kamati ya Usalama na Maadili pamoja na Kamati Kuu vilikuwa vifanyike kati ya Julai 18 na 19, lakini viliahirishwa kutokana na wingi wa watiania, jambo lililosababisha mchakato huo kusogezwa mbele.