…………..
Na Ester Maile Dodoma
Kamati kuu ya chama cha mapinduzi CCM inatarajia kufanya kikao cha maamuzi ya uteuzi wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge, madiwani na uwakilishi ambacho kitafanyika Julai 28 mwaka huu.
Katibu wa itikadi uenezi na Mafunzo wa chama hicho CPA Amos makala ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Taarifa ya kuahirishwa kwa kikao cha kamati kuu ya CCM ambacho kilitakiwa kufanyika Julai 19 , 2025 kwa ajili ya kutangaza majina ya watia nia.
Makala amesema wagombea zaidi ya watu elfu 27 wa udiwani na wagombea ubunge zaidi ya watu elfu 10000 hivo kutokana na idadi hiyo Chama kimejipanga kuchangua viongozi wazurii na kutenda haki.
Aidha CPA Makala “amesema kuna watu wengi wamekuwa wakipiga cm ilikujua sababu ya kuahirishwa kwa kikao hicho kwani wagombea ni wengi hivo chama kinatakiwa kuweza kutulia ili kuchambua wagombea kwa makini “
Hata hivyo baada ya uteuzi wa majina pia Chama Chama Mapinduzi CCM kitatoa ratiba ya kuingia katika kura za maoni.