
MUHIMBILI NA VODACOM KUTOA MATIBABU BILA MALIPO KWA WAKAZI WA TANGA NA KILIMANJARO
::::::: Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania Foundation itafanya kambi maalum ya huduma za uchunguzi na matibabu ya ubingwa bobezi bila malipo kwa wakazi wa mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kuanzia Julai 21 hadi 27, 2025. Kwa wakazi wa mkoa wa Tanga kambi hiyo itafanyika Chuo cha Ualimu Korogwe Julai 21…