Simba Kupoteza Zimbwe JR Ni Pigo Kubwa – Video – Global Publishers



Mchambuzi wa soka nchini, Thomas Mushi, amesema kuwa iwapo mlinzi tegemeo wa Simba SC, Zimbwe JR, ataondoka kwenye kikosi hicho, basi itakuwa pigo kubwa kwa klabu hiyo yenye rekodi kubwa ya mafanikio nchini.

Kauli hiyo imekuja kufuatia kuibuka kwa tetesi zinazoeleza kuwa Zimbwe JR tayari amemalizana na watani wa jadi Yanga SC, na huenda akatangazwa muda wowote kuwa mchezaji wao mpya.

“Kwa kiwango alichonacho Zimbwe JR, ukiondoa mchango wake kwenye safu ya ulinzi ya Simba, pia ni kiongozi kimchezo uwanjani. Kuondoka kwake kutaiathiri Simba ndani na nje ya uwanja,” alisema Mushi.

Ameongeza kuwa Simba SC itahitaji kuingia sokoni haraka kutafuta mbadala wa mchezaji huyo ambaye kwa misimu miwili amekuwa mhimili mkubwa wa beki ya kati ya Wekundu wa Msimbazi.