ASKARI WAWILI WASHIKILIWA KWA MAUAJI YA DEREVA BODABODA

…………..,…..

Na Ester Maile Dodoma 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia Askari polisi wawili  kwa kumjeruhi na kusababisha kifo Cha frank Sanga Mtias mwenye umri wa Miaka 32 ambaye ni  mkulima mkazi wa Mkomwa ,Mtaa wa Kusenha Matumbulu jijini Dodoma .

Hayo ameyasema Kamanda wa jeshi la polisi  Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa polisi Agathon Hyera  Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma amesema tukio ilo limetokea Askari hao wakiwa Doria ya kuzuia uhalifu wakitekeleza majukumu 

Aidha ameeleza kuwa tukio hilo limetokea July 19,2025 majira ya saa 7:30 mchana wakati wakimkamata mwendesha pikipiki aitwaye Mathias Choma mwenye umri wa Miaka 30 Mkazi wa Mpwayungu Wilaya ya Chamwino Dodoma kwa makosa ya usalama barabarani ikiwemo kutovaa helmet, kutokuwa na leseni pamoja na kuendesha pikipiki mbovu.

Pia amefafanua kuwa baada ya kukamatwa ndugu zake walipopata taarifa walikuja kwa wingi baadhi yao wakiwa na siraha za jadi Katika eneo ilo ndipo vurugu ilipoanza ndipo askali mmoja aliamua kufyatua risasi  zilizomjeruhi Frank Sanga Mtias  kwenye paja wa Mguu wa kushoto na kwenye ugoko.