Mwili Wa Mtoto Ramin Wakutwa Kisimani – Global Publishers



Mtoto Ramin

Mtoto Ramin, mwenye umri wa miaka mitatu, ambaye aliripotiwa kupotea na taarifa zake kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, amekutwa akiwa tayari amefariki ndani ya kisima kilichopo nyumbani kwao mkoani Tabora.

Tukio hilo limekuja baada ya juhudi za muda mrefu kutoka kwa familia, majirani na watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao walikuwa wakisaidia kusambaza taarifa za kutoweka kwake.

Kwa mujibu wa baadhi ya ndugu wa familia pamoja na watu wa karibu, mwili wa mtoto huyo uligundulika ndani ya kisima jana Tarehe 20 July 2025.

Jeshi la Polisi mkoani Tabora, kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) Richard Abwao, limetoa ufafanuzi kuhusu kifo cha Mtoto Ramin mwenye umri wa miaka mitatu, ambaye awali aliripotiwa kupotea na taarifa zake kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mwili wa mtoto huyo umekutwa tayari umefariki ndani ya kisima kilichopo nyumbani kwao, mkoani Tabora.