RC BATILDA BURIAN ATOA AGIZO KWA WAKANDARASI MRADI WA UBORESHAJI HUDUMA ZA MAJI KUPITIA HATIFUNGANI YA KIJANI


Na Oscar Assenga,TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amewataka wakandarasi watakaohusika katika utekelezaji wa mradi wa hatifungani ya kijani kwa ajili kuboresha huduma ya maji katika Mkoa wa Tanga kuhakikisha wanautekeleza kwa ufanisi mkubwa na ukamilike kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma lengwa.

RC Batilda aliyasema hayo leo wakati akipokea vifaa ambayo vinakwenda kuboresha huduma za maji katika mkoa wa Tanga na wilaya ya Tanga na Jiji la Tanga ambavyo ni mabomba na viungo yenye urefu wa kilomita 55 na kati ya mabomba yenye urefu wa kilomita 170 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa hati fungaji ya kijani.


Vifaa hivyo vinakwenda kutumika katika kutekeleza na kuendelea mradi wa uboreshaji wa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Tanga katika awamu ya tatu unaogharimu kiasi cha zaidi ya Bilioni 6 ambao utaongeza wigo na fursa ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Maeneo yanayokwenda kutumika na vifaa hivyo katika uboreshaji wa Maji ni Muheza,Pangani na Mkinga ambapo alisema huo ni ubunifu ambao sio mamalaka nyingi za maji mjini zinaweza kwenda wilaya karibia tatu hivyo aliwapongeza kwa kuwa mamlaka ya mfano Tanzania nzima.

“Tunawapongeza sana na tumetayarisha nishani tuwapatie kwa kuendelea kutuheshimisha mkoa wa Tanga katika tasnia ya maji najua mlipewa zawadi siku ya maji katika bara la afrika kama mnatambulika Kimataifa na Afrika na wao kama mkoa watakuwa watu wa ajabu wasipotambuaa mchango wao naa jutihada”Alisema

Alisema kwamba lazima wakandarasi ambao watakaotekeleza mradi huo kuhakikisha wanafanya kazi kwa waledi mkubwa ambao utakuwa chachu ya kukamilika kwa wakati na hivyo wananchi kuweza kunufaika na huduma hiyo muhimu jambo ambalo linawezesha kuondokana na changamoto walizokuwa wanakumbana nazo awali

“Leo hii ni siku muhimu tunapokea mabomba haya na viungio vyake hivyo niwatake wakandarasi wote ambao wanahosuka kwenye utekeleza wa mradi kuhakikisha mradi unatekeleza kwa ufanisi mkubwa na unakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma lengwa”Alisema RC huyo.

Aliongeza kwamba fedha hizo zimetokana na ubunifu mkubwa uliofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) katika kupata hati fungani ya gharamai ya Bilioni 53.12 ambayo imewezea shughuli hizo kuweza kufanyika na kuleta tija kubwa katika utekelezaji wa miradi.

Aidha alitumia fursa hiyo kuhimiza ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo kutokana na upekee wake kwenye bara la ulimwengu kutokana na kwamba uwekezaji wake na waliowekeza hisa kwa sasa wameshaanza kupewa gawio kila kota wanapata gawio.

“Huu ulikuwa ni ubunifu mkubwa na mafanikio yanaonekana kwa mtu mmojammoja na mkoa umekuwa salama kuwa sababu kukosekana kwa maji ni jambo la kiusalama hivyo tuendeee kuhakikisha maeneo yenye uvujaji wa maji mnaendelea kuyazibiti ili kupunguza upotevu wa maji “Alisema RC Balozi Batilda.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa aliipongeza Tanga Uwasa kwa jitihada zao kubwa za kuongeza upatikanaji na ubora wa maji na kuangalia vyanzo vya maji na mipango na mikakakti ya kupanda miti mingi kwa kuwashirikisha wananchi waliopo kwenye vyanzo vya maji ikiwemo kuendelea kutoa vifaa lakini kuwasaidia katika shughui zao mbalimbali ili waendelea kuwa walinzi wazuri na wajue kwamba vyanzo hivyo vinathamani na wanathamni mchango wao katika kuvilimda.

Aliongeza kwamba mkoa huo unathamani mchango unaofanywa na Wizaraa ya maji chini ya Waziri Jumaa Aweso na ameendelea kufanya makubwa Kitaifa na kimkoa ndio maana hata watendaji wa Maji mkoa ikiwemo mameneja hawajamuangusha ndio wamesimama kidete kuelezea umma ilani ya CCM imetekelezwa kwa asilimia 100 na katika miji yetu asilimia 95 ya maji imewezeka kufikiwa.

Awali akizungumza katika halfa hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema kutokana mradi huo anaona mamlaka ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa asilimia 100 kwa muda mfupi ujao hivi sasa wapo asilimia 95 na kukamilika kwa mradi huo asilimia hiyo wameuvuka na mradi huo wanatarajia mpaka utakapofika mwezi Octoba mwaka huu utakuwa umekamilika kama mambo yote yatakwenda sawa.

Alisema kwamba hakuna sababu kwanini yasiende sawasawa kwa leo wamepokea mabomba kontena 11 bado 8 na vitafika kwa muda ambao umewekwa hivyo wanaiona Tanga Uwasa ikitatua shida ya maji katika wilaya hizo nne ambazo ni wilaya ya Tanga,Muheza,Mkinga na Pangani na hawaoni kama kuna shida na wapo wapi tayari hata wakiambiwa wasogee wilaya nyengine ikiwemo Korogwe uwezo wanao kutokana na utalaamu walionao

Aidha alisema kwamba hiyo ni awamu ya nne ya mradi huo na awamu ya kwanza walipanua mtambo wa kusafisha maji na awamu nyengine kusogeza maji kwenye wilaya ambazo wameongezewa na awamu ya tatu ni mkopo kutoka benki ya TIB wakatanua zaidi huduma zao katika awamu tofauti tofauti ikiwemo kurekebisha mitambo ambayo ni ya muda mrefu eneo la usafishaji Maji Mowe na awamu ya nne ni kusambaza huduma ya maji katika maeneo ya miji.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema wana jambo kubwa la kupokea baadhi ya mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa hati fungaji ya kijani ambayo kwa sasa yana kilomita 55 na lengo la mabomba yote yana kilomita 170 ni thamani ya zaidi Bilioni 6.3 .

Alisema mradi huo unalengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji katika wilaya ya Tanga, Mkinga Muheza na Pangani utakapokamilika wananchi 555,000 watanufaika kwa namna mbalimbali wapo ambayo hawajafikiwa na maji watafikiwa na wale ambao miundombinu ulikuwa chakavu itaboresha.

Aidha alisema wanategemea mwisho wa mradi huo hali ya upatikanaji wa maji itakuwa ni nzuri sana lakini pia watajenga miundombinu mikubwa na wanaongeza chanzo cha maji kutoka uwezo wa lita Milioni 42 kwenda Lita Milioni 72 lakini na mtambo wa kusafisha maji kutoka lita milioni 45 hadi Lita Milioni 60 kwa hiyo maji hayo yatasaidia kwenda kwenye hizo wilaya bila shaka yoyote.

Mwisho.