RC CHALAMILA AKUTANA NA MEYA WA JIJI LA DALAS-MAREKANI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 21,2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jiji la Dallas nchini Marekani Mhe Eric Johnson akiwa ameambatana na ujumbe kutoka Jiji hilo ofisini kwake Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao mambo mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo kukuza mahususiano ya kibiashara, uwekezaji, na utalii kwa lengo kukuza uchumi wa pande zote mbili

Aidha ujio wa Meya wa Jiji la Dallas nchini Marekani ni ishara ya kuimarika kwa Diplomasia ya Kimataifa kati ya Tanzania na Marekani vilevile uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza mahususiano ya kidiplomasia ndani na nje ya nchi.