RWEBANGIRA AFUNGUA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA UCHAGUZI NGAZI YA MKOA NA JIMBO WA MIKOA YA RUKWA NA KATAVI

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena Rwebangira leo Tarehe 21 Julai, 2025 amefungua mafunzo kwa Watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Mkoa na Jimbo wa Mikoa ya Rukwa na Katavi katika Ukumbi uliopo katika Ofisi za Mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Mhe.Rwebangira amewasisitiza Watendaji hao kufuatilia mafunzo hayo kwa umakini ili waweze kuelewa kila kinachofundishwa na kutekeleza majukumu yajayo ya Uchaguzi Mkuu wa Ufasaha na weledi.

Mafunzo haya ya siku tatu ambayo yameanza leo tarehe 21 Julai, 2025 yanajumuisha Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa, Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi na Maafisa Ununuzi.