Udiwani viti maalumu, 10 watetea nafasi zao Same

Same. Uchaguzi wa madiwani wa viti maalumu ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Same umekamilika huku madiwani 10 wakifanikiwa kutetea nafasi zao.

Katika uchaguzi huo ambao ulisimamiwa  na Hilary kipingi na Amos  kusakula, zilikuwa tarafa sita ambapo katika kila tarafa wanapaswa kutoka madiwani wawili wa viti maalumu.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi katika Tarafa ya Gonja wagombea walikuwa sita ambapo walioongoza kwa kura ni Happyness Mchome (629) na Christina Kaduma (614).

Tarafa ya Mwembe-Mbaga wagombea pia walikuwa sita na aliyeongoza kwa kura ni Saum Lewanga (749) na Jamila Mdee (669) huku Tarafa ya Ndungu akiongoza Flora Kateberizwe (963) na Veronica Hosein (818)

Katika Tarafa ya Vunta walioongoza ni Janeth Mbwambo (1,462) akifuatia Grace Kiangi (1,147), Tarafa ya Chome -Suji akiongoza Zaina Mghamba (894) na Nashengena Makore (811) huku  Tarafa ya same wakiwa ni Zaina Heshima (1,029) na Happynes Mbonea (621).

Kulingana na matokeo hayo, waliokuwa madiwani ambao wameshindwa kuongoza kwa kura ni Veronica Mnzava (598) kutoka tarafa ya Mwembe-Mbaga na Habiba Irigo(578) kutoka tarafa ya Chome-Suji.