AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA NA MIAKA 30 JELA KWA KULAWITI NA KUBAKA

 ::::::::

Mahakama ya Wilaya ya TANGA mkoani TANGA imemuhukumu CHARLES FELIX (26), mfanyabiashara na mkazi wa DONGE, kifungo cha maisha pamoja na kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya kulawiti na kubaka. 

Hukumu hiyo imetolewa tarehe 22/07/2025 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tanga, Mheshimiwa KOBERO, ambapo ilibainishwa kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mnamo tarehe 28/06/2024 dhidi ya msichana mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa CHUDA. 

Katika ushahidi uliowasilishwa mahakamani, imeelezwa kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti, ambapo tukio hilo liliripotiwa na Sara Luono, mama lishe na mkazi wa Chuda.

 Mshtakiwa alifikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi ya jinai namba 27451 ya mwaka 2024, chini ya vifungu vya sheria vinavyohusiana na makosa ya ubakaji na ulawiti.

 Mahakama ilijiridhisha kuwa upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha usioacha shaka, na hivyo kutoa adhabu ya kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti na kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kubaka dhidi ya mshtakiwa CHARLES FELIX.