Mudathir amaliza utata, atakuwepo Jangwani hadi 2027

Hatimaye kiungo Mzanzibar, Mudathir Yahya Abbas amemaliza utata wa wapi atacheza msimu ujao wa 2025-2026.

Kwa taarifa rasmi ni kwamba, Mudathir ataendelea kuwa kwenye kikosi cha Wananchi hadi mwaka 2027.

Hiyo ni baada ya kiungo huyo kuongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kusali katika kikosi hicho cha Yanga baada ya ule kumalizika mwisho wa msimu wa 2024-2025.

Mudathir alijiunga na Yanga Januari 2023 baada ya kukaa kwa takribani miezi sita bila ya timu yangu alipoachana na Azam FC mwishoni mwa msimu wa 2021-2022. Kumbuka nyota huyo aliitumikia Azam tangu 2012.

Akiwa ndani ya Yanga, kwa misimu miwili na nusu iliyopita kabla ya kuongeza mkataba mpya, amefanikiwa kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu Bara na mengine matatu ya Kombe la FA katika msimu wa 2022-2023, 2023-2024 na 2024-2025, sambamba na Ngao ya Jamii mara moja 2024.

Kuanzia msimu wa 2023-2024, Mudathir mwenye uwezo wa kucheza kiungo mshambuliaji na mkabaji, takwimu zinaonesha amecheza jumla ya mechi 52 za Ligi Kuu Bara akifunga mabao 12 na asisti 7.