Watumishi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamefariki dunia Julai 20, 2025, saa 4 usiku, katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Bwawani Katoro, barabara ya Katoro–Chibingo, Wilaya ya Geita.
Ajali hiyo ilihusisha gari la Serikali aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba STM 3696, mali ya TRA Mwanza, lililoendeshwa na Julius Dismas (31), mkazi wa Mwananchi, Mwanza.
Waliofariki ni: Emmanuel Leonard (33) – Ofisa Forodha, Mwita John (28) – Ofisa Forodha, wote ni wakazi wa Buswelu, Ilemela – Mwanza.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, chanzo cha ajali ni uchovu wa dereva, aliyeshindwa kumudu gari, likapinduka na kusababisha vifo hivyo.
Polisi wanatoa pole kwa familia na kuwataka madereva kuchukua tahadhari, kupumzika kabla ya safari na kuzingatia usalama barabarani.