Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Sunderland leo imezindua mfumo wa mauzo ya jezi ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kwa njia ya mtandao wa internet. Hatua inalenga kuchochea kasi ya mauzo na upatikanaji wa jezi hizo kwa wananchi hususani kipindi hiki kueleka Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) .
Hafla ya uzinduzi wa mfumo huo wa mauzo imefanyika mapema leo jijini Dar es Salaam ikiongozwa na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ sambamba na wadau wengine wa mpango huo wakiwemo wawakilishi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na wawakilishi kutoka wadau wenza huku benki ya NBC ikiwakilishwa na Mkuu wa Idara ya Miamala Bw Mangire Kibanda.
Akizungumza kwenye hafka hiyo Naibu Waziri Mwinjuma, pamoja na kuwapongeza wadau hao kwa mpango huo alionyesha kuunga mkono mikakati mbalimbali inayolenga kuhamasisha matumizi ya jezi ya taifa miongoni mwa wananchi huku akitoa rai kwa wakuu wa taasisi mbalimbali nchini kuangalia uwezekano wa kutenga siku maalum inayotoa fursa kwa wafanyakazi wa taasisi hizo kuvaa jezi za timu ya taifa kama sare maalum ya siku kwa wafanyakazi hao pindi wakiwa kazini.
“Wazo hili ni muhimu sana hususani kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu kwasababu taifa linahitaji kuwa na agenda ya umoja zaidi na michezo ndio kitu kinachoweza kutuunganisha kwa urahisi. Nawaomba sana wakuu wa taasisi mbalimbali hapa nchini wajaribu kuangalia hili suala ikiwezekana sit u kuruhusu bali pia taasisi zenyewe ziweze kuwanunulia jezi hizi wafanyakazi wao tena kwa mfumo huu wa kidigitali kupitia NBC na wadau wake,’’ alisema.
Akifafanua kuhusu mpango huo Bw Kibanda alisema kupitia mfumo wa e-commerce wa benki ya NBC watanzania wanaweza kununua jezi mbalimbali za Taifa Stars bila kutembelea maduka ya mzabuni wa jezi hizo kampuni Sunderland.
“Kupitia mpango huu tunawakaribisha sana wafanyabishara wanaohitaji kufanya biashara ya jezi za Taifa Stars kufanya malipo kwa kuweka fedha kwenye akaunti ya kampuni ya Sunderland iliyopo benki ya NBC au kutembelea matawi yetu na mawakala waliopo sehemu mbalimbali hapa nchini, au pia kutumia huduma zetu za kidigitali ikiwemo NBC Kiganjani na NBC Connect ili waweze kunufaika na huduma ya manunuzi ya jezi hizi kwa ufanisi na haraka hasa kipindi hiki kuelekea michuano ya CHAN’’ alisema.
Zaidi Bw Kibada aliwaomba watanzania wafungue akaunti ya biashara ya benki hiyo ambapo kupitia huduma ya e-commerce wataweza kufanya malipo kupitia kadi zote za kimataifa yaani VISA na Mastercard.
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ (katikati) akikabidhi jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa mmoja wa wadau wa habari wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo wa mauzo ya jezi ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kwa njia ya mtandao wa internet unaoratibiwa kwa ushirikiano na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Sunderland. Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka wadau wa wa mpango huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na wadau wa habari.
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo wa mauzo ya jezi ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kwa njia ya mtandao wa internet unaoratibiwa kwa ushirikiano na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Sunderland. Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka wadau wa wa mpango huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na wadau wa habari.
Mkuu wa Idara ya Miamala wa benki ya NBC Bw Mangire Kibanda (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo wa mauzo ya jezi ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kwa njia ya mtandao wa internet unaoratibiwa kwa ushirikiano na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Sunderland. Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka wadau wa wa mpango huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na wadau wa habari.
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa michezo wakiwemo maofisa wa benki ya NBC wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo wa mauzo ya jezi ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kwa njia ya mtandao wa internet unaoratibiwa kwa ushirikiano na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Sunderland. Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka wadau wa wa mpango huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na wadau wa habari.
Maofisa wa benki ya NBC akiwemo Mkuu wa Idara ya Miamala wa benki ya NBC Bw Mangire Kibanda (katikati) wakifuatilia hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo wa mauzo ya jezi ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kwa njia ya mtandao wa internet unaoratibiwa kwa ushirikiano na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Sunderland. Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka wadau wa wa mpango huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na wadau wa habari.