Mashujaa yamnasa kiungo wa Kagera

MASHUJAA imefanikiwa kunasa saini ya kiungo wa Kagera Sugar, Samwel Onditi kwa kumpa mkataba wa miaka miwili, mabosi wa klabu hiyo wamethibisha.

Onditi aliyekuwa mmoja ya mastaa walioshuka daraja na timu hiyo kutokana na kumaliza nafasi ya 15 katika msimamo wa timu 16 sambamba na KenGold.

Kabla ya kuitumikia Kagera, Onditi amewahi kukipiga pia timu za Singida Big Stars enzi ikifahamika kama Ihefu na Geita Gold.

Akizungumza na Mwanaspoti mmoja wa viongozi wa Mashujaa ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa, ni kweli wamekamilisha usajili na kiungo huyo.

“Tumekamilisha usajili kwa kumalizana na Onditi ni kiungo mzuri kijana mwenye nguvu ambaye tuliona kuna nafasi ya kumpata na tukamalizana naye.

“Kwa sasa tumemaliza usajili rasmi labda itokee dharura sana, tunachosubiri ni kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya ili mwalimu akatutengenezee timu Bora kwa msimu ujao.”

Mashujaa inajipanga kwenda kwenye maandalizi ya msimu ujao.