Katika kuadhimisha robo karne ya uwepo wake nchini na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake, Vodacom Tanzania PLC imeanzisha kampeni kabambe ya nchi nzima ijulikanayo kama “Tupo Nawe, Tena na Tena.” Kampeni hii, itakayodumu kwa miezi minne, inalenga kuwakumbusha Watanzania jinsi Vodacom ilivyokuwa nao bega kwa bega katika kila hatua ya maisha yao.
Kuanzia enzi za mawasiliano ya kawaida hadi sasa ambapo teknolojia ya dijitali inatawala, ikijumuisha huduma za M-Pesa, 5G, afya mtandaoni, na elimu kwa njia ya simu, Vodacom imekuwa mstari wa mbele. Kupitia kampeni hii, Vodacom inatoa shukrani za dhati kwa wateja wake wote na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora na ubunifu kwa miaka mingi ijayo, ikithibitisha nafasi yake kama mtandao unaoaminika zaidi nchini.