Pamba, Kadikilo bado kidogo tu

PAMBA Jiji imekamilisha dili la usajili wa beki wa Fountain Gate, Amos Kadikilo, huku kiongozi wa klabu hiyo akifichua kila kitu kilichofanyika hadi sasa.

Kikosi hicho cha Pamba kilipanda daraja msimu uliomalizika na kufanikiwa kumaliza nafasi ya 11, ikiwa na pointi 34.

Kadikilo aliyewahi kucheza Geita Gold kwa misimu miwili na kuifungia mabao manne kabla ya kutimkia Fountain Gate aliyoitumikia kwa misimu miwili akifunga mabao mawili msimu ulioisha.

Akizungumza na Mwanaspoti, mmoja wa viongozi alisema hadi sasa Pamba imeshafikia 100% ya makubaliano kati ya pande zote mbili, ingawa kuna mambo madogo yaliyochelewesha dili hilo.

“Nadhani mchezaji alikuwa na mambo aliyokuwa akiyamalizia na timu yake ya msimu uliomalizika ndio maana tumechelewa kidogo kumsajili, ila tumekamilisha makubaliano ndani ya siku mbili zilizopita.

“Licha ya kwamba hajacheza sana kule alikotoka lakini kwetu tuna imani naye kwa sababu nimewahi kumuona katika timu alizotoka hivyo hatuna shaka naye.” alisema kiongozi huyo.

“Tulifanya mazungumzo na mchezaji mwenyewe kwa sababu alishamalizana na klabu aliyokuwa anaitumikia.”

Fountain ilinusurika kushuka daraja baada ya kumaliza katika nafasi ya 14,l akini ilisalia Ligi Kuu kwa kuichapa Stand United 3-1 katika playoffs.