KIPIGO cha pointi 106-22 kutoka kwa Pazi, kimeifanya Mgulani JKT kujiweka katika wakati mgumu wa kubakia katika Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (BDL) mwakani.
Mgulani ilipata kipigo hicho kwenye Uwanja wa Donbosco Upanga kutokana na kufungwa michezo yote 10 huku ikibakiza mitano.
Timu hiyo imekusanya pointi 10 ikiwa ni kutokana na kanuni zinazoipa pointi moja inayofungwa, huku inayoshinda inapata mbili.
Inaelezwa Mgulani imefanya vibaya kutokana na kutokuwa na wachezaji wanaoweza kutoa ushindani katika ligi hiyo.
Katika mchezo huo, Pazi iliongoza katika robo zote kwa pointi 24-6, 23-9, 29-2 na 30-5.
Soro Godfrey wa Pazi aliongoza kwa kufunga pointi 20, huku Yasini Shomari wa Mgulani JKT akifunga pointi 14.