RAIS MWINYI AWASILI LUPASO KUHUDHURIA IBADA MAALUM YA KUMBUKUMBU MIAKA MITANO YA HAYATI MKAPA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Zanzibar leo, tarehe 23 Julai 2025, na kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Nachingwea tayari kuelekea Lupaso, Mtwara, kuhudhuria Ibada Maalum ya Kumbukumbu ya Miaka Mitano ya Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa.

Alipowasili alipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala, pamoja na Viongozi mbalimbali wa wa Serikali na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.