Trump Afikia Makubaliano Ya Kibiashara Na Japan – Global Publishers



Rais wa Marekani, Donald Trump
Habari hii imeandikwa na Glory Sisty.

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kukamilika kwa makubaliano ya kibiashara kati ya Marekani na Japan, yakihusisha sekta za kilimo, viwanda, na huduma za kidijitali.

Makubaliano hayo, ambayo yalianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2019, sasa yamekamilishwa rasmi katika muhula wa pili wa utawala wa Trump, yakilenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.

Trump ameeleza kuwa makubaliano hayo ni ushindi kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili, na yatafungua milango mipya ya ushirikiano katika teknolojia, usambazaji wa bidhaa, na ajira.