Kuelekea NBC Dodoma Marathon: Benki ya NBC Yakabidhi Pikipiki 10 Kwa jeshi la Polisi Kuimarisha Usalama, Yakabidhi ‘Kits’ kwa Mkuu wa Mkoa Dodoma

 Waandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo wamekabidhi pikipiki 10 zenye thamani ya sh mil 28 kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuunga mkono jitihada za mkoa huo katika kuboresha musuala ya usalama na kukabiliana na uhalifu hususani kipindi kuelekea mbio za NBC Dodoma Marathon…

Read More

Orphanage Centre Yafurahia Ujio wa BITTECH na KMC

KATIKA mwendelezo wa kurejesha kwenye jamii, leo hii Kampuni ya Bittech kwa kushirikiana na klabu ya ligi kuu ya Tanzania KMC waliungana pamoja na kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto wa kituo hicho. Bittech na KMC waliona kuna umuhimu mkubwa kabisa wa kufika katika kituo hicho ambacho kinapatikana Mburahati Maziwa ambapo waliweza kutoa…

Read More

Hospitali ya Wilaya Karatu yaondoa adha kwa wananchi

Karatu. Kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karatu umesaidia kuondoa adha ya baadhi ya wananchi wilayani humo, waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma. Hayo yameelezwa leo Jumanne Julai 24, 2025 na baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenan Kihongosi wilayani humo kukagua shughuli mbalimbali…

Read More

Waeleza machungu wanayopitia baada ya ajali ya moto Morogoro

Morogoro. Ikiwa imepita miezi minne tangu kutokea kwa tukio la ajali ya moto uliounguza karakana na vibanda 16 vya kutengeneza na kuuza samani za ndani, Mtaa wa Ngoto Manispaa ya Morogoro waathirika wa tukio hilo wameanza upya biashara wakitumia vifaa na mashine duni. Mafundi selemala na wafanyabiashara hao wamelazimika kutumia vifaa na mashine hizo duni…

Read More

Siasa za uchaguzi zatawala ibada ya kumuaga Mama Makete

Dar es Salaam. Ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Kinondoni, Anna Hangaya maarufu Mama Makete imetawaliwa na vimbwanga, kicheko na siasa za michakato ya uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hicho. Ni jambo ambalo kwa hali ya kawaida usingedhania, pengine kungetawala kilio…

Read More

Stamico yapewa leseni ya utafiti na uchimbaji madini adimu

Morogoro: Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amelitaka Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kuharakisha mchakato wa uendelezaji wa leseni waliyokabidhiwa ya utafiti na uchimbaji madini adimu na muhimu katika kilima cha Wigu kilichopo Kijiji cha Sesenga Tarafa ya Bwakila, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. Mavunde ametoa agizo hilo wakati wa hafla  ya makabidhiano ya leseni…

Read More