…………….
Na Ester Maile Dodoma
Siku ya Mashujaa ni siku ya kumbukumbu ya wa Tanzania waliopoteza maisha ,nguvu zao na kutoa sadaka zao kwa ajili ya uhuru ,amani na maendeleo ya Taifa letu.
Hayo yamebainishwa hii leo 24 Julai 2025 Dodoma, na Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Dotto mashaka Biteko wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho hayo yatakayo fanyika kesho 25Julai 2025 katika uwanja na Mnara wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali ,Mtumba jijini Dodoma.
Aidha amesema Mgeni rasm katika Maadjimisho hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo saa 6:00 usiku wa 24Julai ,2025 mwenge wa kumbukumbu ya Mashujaa utawashwa Rasmi na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Sitaki Senyamule kwaniaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kuashiria kuanza kwa maombolezo ya Mashujaa wetu.