Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na UNDP, imezindua nyaraka tatu muhimu za usimamizi wa maafa katika Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
✅ Nyaraka zilizozinduliwa:
Mpango wa Kujiandaa na kukabiliana na maafa ya Wilaya (D-EPRP)

Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya Maafa (D-DRRS)
Ripoti ya Tathmini ya Vihatarishi, Uwezekano wa Kutokea na Uwezo wa kukbailian na maafa (RVCA)
📅 Uzinduzi umefanyika tarehe 23 Julai 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wananchi.
🎙️ Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Nyakia Chirukile:
“Hii ni hatua muhimu kujenga mfumo wa utayari dhidi ya majanga kama mafuriko.”
🎙️ Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hosea Ndagalla, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa OWM:
“Ni utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya 2022.”
🎙️ UNDP Tanzania kupitia Bw. Godfrey Mulisa:
“Mpango huu ni sehemu ya kusaidia jamii kujenga upya maisha yao na kuwa imara zaidi.”
Wadau wa maendeleo wametoa pongezi na kuahidi kushiriki kikamilifu kutekeleza mpango huu.
🟢 #Maafa2025 #Sumbawanga #UtayariDhidiYaMajanga #UNDP #OWM