CCM YAITISHA MKUTANO KIDIGITALI

………… 

Na Ester Maile Dodoma 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitisha mkutano mkuu maalum kwa njia ya mtandao kesho Julai 26 huku ajenda kuu ikitajwa kuwa ni marekebisho madogo ya Katiba.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi na Mafunzo Amos Makala, amesema hayo leo Julai 25, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maabdalizi ya mkutano huo mkuu maalum.

Makala, amesema kumekuwepo na maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao.

“Ajenda ya mkutano huu maalum ni moja tuu ambayo ni mabadiliko madogo ya katiba ambayo yawezikufanywa na kilao chochote zaidi ya mkutano mkuu.

“Mabadiliko ya katiba hayawezi kufanywa na NEC,Kamati Kuu wala vikao vya Sekretarieti bali ni wenye katiba yao ambao ni mkutano mkuu”,amesema.

Amesema kwamujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi CCM, inawaruhusu kufanya mkutano mkuu maalum kwa njia ya mtandao pale wanapoona inafaa.

Aidha amesema hadi sasa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kwa mara ya kwanza watu watakwenda kushuhudi chama hicho kikifanya mkutano mkuu kwa njia ya mtandao.

“Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100, wilaya zipo tayari mikoa yote ipo tayari Sekretarieti tunaendelea na maandalizi ili kufanikisha mkutano huu mkuu maalum ambao utatanguliwa na vikao vya kamati kuu na halmshauri kuu ya CCM,”amesema