Marekebisho ya Katiba CCM kufanyika kwa njia ya mtandao kesho

Dodoma. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeita mkutano Mkuu Maalumu kesho Jumamosi Julai 26, 2025.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla amewaambia waandishi wa habari kuwa lengo la mkutano huo ni kufanya marekebisho madogo ya Katiba ya chama hicho.

Mkutano huo utafanyika kwa njia ya mtandao na tayari Makalla amesema maandalizi yote yamekamilika.

“Nimepokea simu nyingi kutoka kwa watu na kwenye mitandao watu wameandika mambo mengi, nawathibitishia kuwa kesho tutakuwa na mkutano Mkuu Maalumu ambao utafanyika kwa njia ya mtandao,” amesema Makalla.

Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake.