RC Chalamila Awaomba Radhi Watumiaji Wa Mwendokasi – Global Publishers



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaomba radhi watumiaji wa magari ya Mwendokasi kwa adha wanazokumbana nazo katika kipindi hiki, akieleza kuwa serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto zilizopo ili kuboresha huduma hiyo muhimu kwa wakazi wa jiji.