Mbeya. Watu kadhaa ambao bado idadi yao haijajulikana wanahofiwa kufariki dunia katika ajali maeneo ya mteremko wa Nzovwe hadi kwenye daraja la Iyunga kunakoendelea ujenzi wa barabara ya njia nne jijini Mbeya ikihusisha magari matano.
Ajali hiyo imetokea leo Julai 27, ambapo Mwananchi Digital imefika katika maeneo hayo na kushuhudia Jeshi la Polisi, Zimamoto na wananchi wakisaidia kuokoa baadhi ya majeruhi na kutoa miili ya waliofariki dunia.
Ajali ya kwanza imehusisha gari la abiria linalofanya safari zake Mbalizi – Nsalaga, lori na tipa kwa upande wa eneo la Nzovwe.
Kwa upande wa eneo la Iyunga, imehusisha gari aina ya Coasta inayofanya safari kati ya Mbalizi – Standi Kuu, Lori lililokuwa na shehena ya saruji na mengineyo ambayo hayakutambulika haraka.
Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi.