MATUKIO KATIKA PICHA; BALOZI DKT. NCHIMBI AKIZUNGUMZA NA MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na kuagana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango, baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa.


Mkutano huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ulifanyika kwa njia ya mtandao katika Ukumbi wa Mikutano wa NEC, Makao Makuu ya CCM, Jumamosi tarehe 26 Julai 2025, jijini Dodoma.

Wengine pichani, ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, ambao ni, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko (kulia) pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe Zubeir Ali Maulid.