HALMASHAURI YA MERU YAJIVUANIA BOOST KUWEZESHA UTEKELEZAJI WA SERA YA ELIMU

Kupitia Program ya BOOST, Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha, imepokea jumla ya Sh. Bilioni 2 na milioni 71 ambayo imewezesha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Elimu ya Awali na Msingi.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Zainabu Makwinya kati ya fedha hizo Sh. Milioni 332 zinawezesha ujenzi wa Shule ya Msingi kwenye Shule ya Sekondari, ikiwa ni miongoni mwa Shule zinazojengwa nchi nzima kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Elimu, kwa kuzingatia Elimu ya lazima sasa ni miaka kumi.

“Shule hii si tu kwamba itakuwa ya mfano bali inawakilisha taswira ya elimu na ujuzi unaohitaji kulingana na mahitaji ya Karne ya 21 na kufungua fursa kwa kizazi kijacho,” amesema.

Amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania imedhamiria Kuboresha miundombinu ya kimkakati kuwezesha vijana kuwa na maarifa na stadi zitakazowawezesha kujiajiri na kuajiriwa katika nyanja mbalimbali Kitaifa na Kimataifa.