MAJALIWA ASHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA ACTIF 2025, GRENADA

:::::

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 28, 2025 ameshiriki katika ufunguzi wa Jukwaa la nne wa Kibiashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (Afri-Caribbean Trade and Investment Forum – ACTIF 2025) mjini St. George’s, nchini Grenada, Julai 28,2025 ambapo alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkutano huo unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa ya Afrika na visiwa vya Karibiani umehudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka maeneo hayo.