Ajali ya moto imetokea katika eneo la Sinza Superstar, barabara ya Sam Nujoma Jijini Dar es Salaam ikihusisha gari aina ya Toyota Vanguard lenye namba za usajili DTG 215.
Kwa maelezo kutoka kwa mnusurika wa ajali hiyo ambaye ni mmiliki wa gari hilo, moto ulianza kwenye boneti ya gari na haraka ulienea.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo la tukio mara baada ya kupokea taarifa, lakini licha ya juhudi zao, hawakuweza kuokoa gari hilo.
Hakuna taarifa ya watu kujeruhiwa vibaya au vifo katika tukio hili. Hali ya mnusurika ni shwari.