Baba Levo apenya mchujo Kamati Kuu CCM Kigoma

Dar es Salaam. Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Clayton Chiponda ‘Babalevo’ ni miongoni mwa watiania sita waliopenya katika chujio la Kamati Kuu ya chama hicho, sasa anasubiri kura za maoni kutoka kwa wajumbe agombee ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini.

Sambamba naye, wengine waliopenya ni Baruani Muhuza, Kirumbe Ng’enda, Ahmad Sovu, Maulid Kikondo na Moses Basira.

Hayo yameelezwa leo, Jumanne Julai 29, 2025 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla alipozungumza na wanahabari jijini Dodoma.

Kwa upande wa Kakonko, amesema watiania saba wameteuliwa ambao ni Aloyce Kamamba, Amos Gwegwenyenza, Dk Kagoma Kamana, Alan Mbano, Rosemary Luhinda, Modest Apolinary na Nsakila Kabembe.

Katika Jimbo la Muhambwe, amewataja walioteuliwa ni saba ambao ni Florence Samizi, Jamal Tamimu, Dickson Bidebeli, Anderson Kabuko, Geradina Kabululu, Julius Thomas na Nduhibusa Mapigano.

Makalla amewataja sita walioteuliwa Kasulu Mjini ni Profesa Joyce Ndalichako, David Doya, Fadhil Ngezi, Magreth Kilenza, Mteule Mkombo na Patrick Zugimbasha.

Aidha, katika Jimbo la Kasulu Vijijini, wameteuliwa sita ambao ni Agustine Hole, Agripina Buyongela, Edibili Kimnyoma, Emmanuel Msasa, Seleman Wandwi na Shukurani Mpaganyi.

Kwa upande wa Buhigwe amesema wameteuliwa sita ambao ni Mtakimanzi Yusuph, Elias Kayandabila, Dk Yusilda Kabujanja, Profesa Pius Yanda, Casian Mbagije, Eliadory Kavyejuri, huku Kigoma Kaskazini wakiteuliwa Peter Serukamba, Assa Makanika, Godfrey Lusimbi, Maseri Tarinega, Shaaban Mtunda na Athuman Bakene.

Kigoma Kusini, amesema wameteuliwa saba ambao ni Nuru Kashakari, Yasinta Kafulila, Nashon Byanguze, January Kizito, Peter Nyabakari, Majaliwa Zuberi na Dk Rajab Abed.