Na Seif Mangwangi, Arusha
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Kwa upande wa Tanzania Bara kimeteua majina nane kwa Mkoa wa Arusha ya wagombea nafasi za Ubunge wa Viti Maalum.
Miongoni mwa majina hayo limo jina la Chiku Athuman Issa ambaye ni Meneja wa zamani wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini.
Aidha Chiku Athumani Issa ni Mjumbe wa kamati ya Uchumi, Mpango, Fedha UWT Taifa,Mjumbe wa Mkutano UWT Taifa .Pia ni Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji wilaya Arusha jiji.