Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ameteuliwa kuwa mtiania pekee katika Jimbo la Bukombe baada ya makada wengine kutojitokeza kutia nia.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla leo Jumanne Julai 29, 2025 wakati akitangaza majina ya walioteuliwa na CCM kwenda hatua inayofuata ya kura za maoni.
Makalla amesema kwa Mkoa wa Geita mbali na Bukombe, Jimbo la Busanda walioteuliwa ni wanne ambao ni Laulecia Bukwimba, Dk Busanda Busanda, Japhari Seif na Zadoki Mathias.
Jimbo la Chato Kaskazini walioteuliwa ni watano ambao ni Colnely Maghembe, Medard Kalemani, Francis Fredrick, Simon Bulengaja, Cosmas Makongo.
“Jimbo la Chato Kusini, wametuliwa wagombea wanne ambao ni Paschal Lutandula, Deodedith Katwale, Philbert Buhula na Silvester Simon,” amesema.
Makalla amesema Jimbo la Geita Mjini, walioteuliwa ni watano ambao ni Chacha Wambura, Cosntatine Kanyasu, Upende Peneza, Gabriel Robert na John Saulo.
Jimbo la Geita walioteuliwa ni wanne akiwamo Emmanuel Shelendi, Msukumu Kasheku, Patrick Malogomi, Sophia Mashala.
Jimb la Katoro, walioteuliwa ni watano, Tumaini Magesa, Kija Ntemi, Esther Ng’ome, Mathia Lupuga na Simon marandu.
Mbongwe, Agustino Masele, Fargason Masasi, Patrick Msafi na Isaya Kingi. Jimbo la Nyang’wale walioteuliwa ni Evarist Ndikilo, Hussein Ammar, Thomas Dibush na Joyce Kakumbi.
Endelea kufuatilia Mwananchi.