ZAHARA MICHUZI ACHOMOZA UBUNGE VITI MAALUM TABORA

:::::

KAMATI Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa imempitisha Mkurugenzi Mtendaji (DED) katika Halmashauri tatu tofauti, Meatu (Simiyu), Ifakara (Morogoro), na Geita (Geita Mjini)

Bi. Zahra Muhidin Michuzi katika uteuzi wa awali wa wagombea nafasi za ubunge kupitia Viti Maalumu Wanawake katika Mkoa wa Tabora.

Zahra Michuzi anachuana na wagombea nane (8) akiwemo Aziza Sleyum ALLY, Jaqueline Kainja ANDREW, Christina Solomon MNDEME, Zuena Mohamed YUSUPH, Dkt. Bayoum Awadhi KIGWANGALA, Mkuwe Abdul ISSALE na Rebeka Joseph KASHINDY.

Aidha Zahra anajivunia rekodi ya uongozi ulioleta mabadiliko halisi katika maeneo aliyohudumu. Kabla ya kupandishwa cheo kuwa DED, aliwahi pia kuwa Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) katika Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, nafasi aliyoitumikia kwa weledi na kujenga imani kwa viongozi na wananchi.

Kwa kuingia kwake kwenye siasa, hasa katika nafasi ya uwakilishi wa wanawake kupitia UWT, Zahara analeta pamoja uzoefu wa kiutawala, usimamizi wa miradi ya maendeleo, na uelewa wa changamoto halisi zinazowakabili wanawake na jamii kwa ujumla katika mkoa wa Tabora na Tanzania nzima.

Wadadisi wa siasa wanaona uamuzi wa Zahara kama hatua ya kuhamasisha wanawake waliobobea katika sekta ya umma kushiriki moja kwa moja katika uundaji wa sera, hasa zile zinazolenga ustawi wa wanawake, vijana, na makundi maalum.