LIVE: Kesi ya Lissu ikiunguruma mahakamani, hatima kujulikana leo

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, leo Jumatano, Julai 30, 2025 amefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, huku Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) akitarajiwa kutoa hatima uhamishwaji wa kesi hiyo kwenda Mahakama Kuu.


Kesi ya Lissu ikiunguruma mahakamani, hatima kujulikana

Kesi hiyo imefunguliwa mahakamani hapo kwa ajili ya uchunguzi wa awali kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu ambayo ndio ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya uhaini, baada ya taratibu za msingi kukamilika ukiwemo upelelezi.

Endelea kufuatilia Mwananchi.