Mweyekiti wa Tume Huruya Uchaguzi Jaji Jacob Mwambegele amesema tume yake imepania kuelimisha wapigakura nini cha kufanya kabla ya siku ya kupiga kura na imeteua taasisi na asasi za kiraia za ndani na nje ya nchi kutoa elimu ya mpiga kura na kusimamia uchaguzi mkuu ujao.
Jaji Mwambegele aliyasema hayo leo Julai 30, 2025 alipokutana na Taasisi na Asasi za Kiraia jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwa kuzingatia kifungu cha 30 (1) (g)(h) na (i) cha Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi Na.2 ya mwaka 2024, tume inayo waibu wa kutoa elimu ya mpiga kura nchini, kuratibu na kusimamia taasisi na na asasi zinazotoa elimu ya mpiga kura na kualika na kusajili waangalizi wa uchaguzi.
“Katika kutekelza jukumu hilo tume kwa upande wake imejipanga kutoa elimu hiyo kwa njia mbalimbali ambazo ni Pamoja na vyombo vya Habari, Mitandao ya Kijamii, Machapisho, mikutano na wadau kama tunavyofanya leo haapa, kushiriki katika maonesho na matamasha, kutumia gari la elimu ya Mpiga Kura la Tume na magari ya matangazo kwenye halmashauri kote nchini,” amesema Jaji Mwambegele.
Amebainisha kuwa tayari tume imetoa kibali cha kutoa elimu kwa mpiga kura kwa taasisi na asasi za kiraia 164 kwa ajili ya kutoa elimu kwa mpiga kura wakati wa kupindi cha hiki cha uchaguzi.
Alisema vile vile jumla ya taasisi na asasi 76 za ndani na 12 za kimataifa zimepata vibali za uangalizi wa uchaguzi.
Jaji Mwambegele ameahidi tume yake kusimamia uchaguzi huo kwa njia ya haki, huru na wazi na kuwa wa kuaminika kwa kuweka mazingira sawa ya ushindani kwa wagombea wa vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki.