AMINA GOOD AONGOZA KWA KURA 421 KATI YA KURA 768.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Amo Foundation Tanzania Amina Good Said ameongoza kwa kura 421 kati ya kura 768.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa matokeo hayo na Msimamizi wa uchaguzi huo katika Mkutano Mkuu Maalum wa Mkoa wa Dar es salaam Amina, amewashukuru wapiga kura kwa kuwa na imani naye na kuhakikisha wanawake wanashiriki vema kutafuta ushindi wa kura za uchaguzi Mkuu kwa nafasi za Urais, Wabunge na Madiwani.

Ameongeza kuwa ili imani waliyompa itimie ni lazima kushinda majimbo na kata zote za mkoa wa Dar es salaam na Chama Cha Mapinduzi kishinde katika majimbo mengi ili nafasi za viti maalum zipatikane nyingi.

Amebainisha kuwa kazi ya maendeleo kwa wanawake itaendelea kuhakikisha wanaimarika kiuchumi, kupitia vikundi na makundi mbalimbali katika jamii.

Ameongeza kuwa kwa uchaguzi wa kura za maini hatua ya awali umemalizika anawaomba wanawake wote waliomuunga mkono na wale wa makundi mengine kuvunja makundi na kubaki na kundi la Ushindi la CCM.

Uchaguzi wa kura za maoni za viti maalum Mkoa wa Dar es salam ulishirikisha wagombea tisa wanawake ambao wote wamekubali matokeo na kuahidi kutafuta kura za Chama Cha Mapinduzi.