CCM YAMPITISHA DEOGRATIUS SENI KUWANIA UDIWANI

:::::::

 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia kikao chake kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 28 Julai 2025, imempitisha Deogratius Seni Kata Shagihilu mkoa wa shinyanga kuwa miongoni mwa wanachama walioteuliwa kushiriki kura za maoni kwa nafasi ya udiwani kupitia chama cha Mapindunzi CCM Kata ya Shagihilu.

Seni, ambaye ni fundi wa mitambo ya upepo na mhasibu wa Ndoleleji Mission, ana elimu ya ufundi kutoka Chuo cha Windmills Matanda (Shy) na elimu ya biashara kutoka Chuo cha Baraka nchini Kenya. Amewahi pia kuhudumu kama Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) katika kata hiyo.

Kupitishwa kwake katika hatua hii ya mchujo ni ishara ya kuaminiwa kwake ndani ya chama, na sasa atasubiri kupigiwa kura na wajumbe wa CCM Kata ya Shagihilu ili kuwania nafasi ya kuwa mgombea rasmi wa chama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.