:::::::
Wafanyabiashara na wakazi wa maeneo ya Bwiro na Bukondo Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza wametoa shukrani za dhati kwa Serikali kufuatia kuwajengea maegesho ya kivuko pande zote mbili za Bwiro na Bukondo ikiwa ni maandalizi ya ujio wa kivuko kipya cha MV. BUKONDO.
Kivuko cha MV. BUKONDO tayari kimefikia zaidi ya asilimia 94% ya
ujenzi wake na kitakuwa na tani 100, uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 kitakapokamilika. .