
Bahati mbaya ya Inonga ni nyakati, fedha
HENOCK Inonga aliondoka nchini mwaka jana kwenda Morocco kujiunga na AS FAR huku akiwa mchezaji ambaye hakuna klabu ya Tanzania haikutamani kuwa naye. Simba ilimruhusu kishingo upande aende Morocco kwa vile alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi chao lakini hata watani zao wa jadi Yanga bila shaka wasingeweza kuchezea fursa ya kutomsajili iwapo angeamua kujiunga nao….