
KONA YA MALOTO: Karata za urais 2030 CCM, zinachezwa 2025
Mayowe na miluzi ni mingi kuzunguka uteuzi wa wagombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Taarifa za waliokatwa na waliopenya zinatawala mitandao ya kijamii. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, ameshatoa tamko kuwa hakuna ambaye ameshakatwa. Zipo taarifa zinasambaa pia kuhusu waliotangazwa kukatwa, kisha kurejeshwa….