
Mwisho wa enzi Profesa Lipumba kuisaka Ikulu
Wakati mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu ukikamilika ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), Mwananchi imethibitishiwa kwamba mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba hatogombea tena urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu kuanza kwa chaguzi katika mfumo wa vyama vingi, Profesa Lipumba amegombea urais mara tano kuanzia mwaka 1995, 2000, 2005, 2010…